Mchango kwa Kituo cha Watoto Yatima Cha CHAKUWAMA

Mchango kwa Kituo cha Watoto Yatima Cha CHAKUWAMA

Share via

Salaam ndugu;

Tunaomba tuchukue fursa hii kukushirikisha jambo muhimu kweli. Tunapenda kukushirikisha katika Shukrani Maalumu ambayo tunatarajia kufanya Siku ya Jumatatu jioni tarehe 05/12/2016 ambayo ni siku yetu ya Kuzaliwa. Siku hii ninatarajia Kutembelea Kituo cha Watoto Yatima Cha CHAKUWAMA kilichopo Pale Sinza Mori. (Mkabala na mtaa wa Meeda- Pia Ni Rahisi ukiingia Kutokea service road ya Lufungira Upande wa Kwa Kakobe kuelekea Sinza- Panajulikana na pako barabarani)

Kituo kina watoto 90 ambao watoto 50 wote wanasoma, wengine 40 bado ni wadogo. Kwa mujibu wa waendeshaji wa kituo hiki ni kuwa, kuna mahitaji mengi ila mahitaji ya muhimu wanayohitaji kwa sasa ni pampers na maziwa ya unga. Wahitaji wa pampers ni watoto miezi sita hadi miaka mitatu. Hivyo basi Kwa uwezo na nguvu zetu peke yetu hatuwezi kuwasaidia na kumaliza mahitaji yao ila kwa umoja wetu tunaweza kuwasaidia kidogo. Hivyo Kwa unyenyekevu tunaomba mtuunge Mkono kujumuika nasi kuwawasilishia sadaka zetu ndogo na Kukata keki Ya Birthday Pamoja nao kuanzia saa kumi na mmoja Jioni (5.00PM) kituoni hapo.

Tunatanguliza shukrani zetu za dhati kwako, tunakuomba tuungane pamoja katika kufanikisha hili.

Ni sisi Mujuni Baitani & Mwasapi Kihongosi

Kwa mawasiliano Zaidi: +255713823509/ 755100298 (Mujuni); Mwasapi (0752030032)

Kuzungumza na ungozi wa CHAKUWAMA

Venue location in map

Organizer information

When & where

Sinza Mori,

Thu 01 to Mon 05, December 2016

3:00am to 3:00am

Add to my calendar

Google calendar

#Past event